WELCOME TO THE GOVERNMENT OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 8031 DAR ES SALAAM, E-MAIL: maelezo@habari.go.tz/maelezopress@yahoo.com FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/Habari Maelezo, FOLLOW US ON TWITTER >>> @Habari_Maelezo.KARIBUNI

Monday, 25 July 2016

WHO YATOA MAFUNZO KWA WATAALAM WA AFYA KUTOKA NCHI 14 ZA BARA LA AFRIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva - Switzarland,  Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kwa lengo kuwajengea uwezo watalaam kuhusu ujazaji wa taarifa  kuhusu sababu ya kifo cha mgonjwa pindi wanapojaza cheti cha kifo (Death Certificate).Washiriki  wa Mafunzo hayo ya Siku mbili watakua na jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi wanazotoka kuhusu mfumo huo.
 Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua  sababu ya kifo cha mgonjwa utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo. 
Mtakwimu kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania, Zambia na Cameroon wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania na Malawi wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya mwisho ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.

Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Dkt. Samuel M. Nyantahe


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Julai, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Samuel M. Nyantahe alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Dkt. Samuel M. Nyantahe anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ambaye amejiuzulu wadhifa huo.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
25 Julai, 2016

Watanzania waaswa kudumisha amani iliyopo nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwaasa watanzania kudumisha amani ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa wetu kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili  Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Magufuli katika harakati za kuijenga Tanzania mpya.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa  Dkt.Ali Mohamedi Shein akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kusisitiza kuhusu umuhimu wa watanzania kuenzi amani iliyoasisiwa na wazee wetu na kuacha kushiriki katika vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samweli Malechela akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kumshukuru kwa kusimamia na kutekeleza ahadi zilizowahi kutolewa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo kuhamishia serikali Mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kumuahidi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa maagizo ya kuitaka Serikali ihamie mjini Dodoma.

Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa baada ya kuwekwa kwa silaha za asili za mashujaa na maua

Baadhi ya wananchi wakifuatilia shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.
(Picha na Hassan Silayo)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiweka silaha za asili kwenye Mnara wa Mashujaa leo Mkoani Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania
(Picha na Ikulu)
Na: Immaculate Makilika- Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa watanzania kudumisha amani iliyopo ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa mbalimbali kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.

Akizungumza leo, wakati akihutubia wananchi mara baada ya kumaliza shughuli za maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa  iliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.

Rais Magufuli alisema kuwa maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa  ni muhimu kwa vile watu hao walijotoa kwa ajili ya kulitetea taifa.

“Wakati tunawakumbuka waliotangulia mbele za haki, sisi tuliobaki tudumishe amani hii, kama ambavyo wao waliotutangulia hawakujali dini zao bali taifa hili” alisema Rais Magufuli.

Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania imebaki kuwa kisiwa cha amani, na amani hiyo isichezwe  bali ijengwe na kudumishwa kwa umoja na mshikimamano ili kusaidia kuitangaza nchi zaidi.

Aidha, viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Ali Mohamedi Shein, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili  Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samweli Malecela nao wapewa fursa ya kuzungumza na wananchi kuhusu maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.

Viongozi hao, wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani iliyopo na kusema kuwa ni jukumu la wananchi  wote kuhakikisha  hawashiriki katika vitendo vitakavyosababisha   uvunjifu wa amani.

Ambapo, waliwataka wananchi kuwaombea Mashujaa wote waliofariki katika vita mbalimbali wakiwa  katika  harakati za kulifanya Taifa la Tanzania kuwa huru.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, alisema kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa agizo la Rais la kuitaka Serikali kuhamia mjini Dodoma.

“Nahamia Dodoma mwezi wa tisa,na nitakapohamia mawaziri wote lazima wanifuate. Katika hili nitasimamia kwa nguvu zote” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Awali, Mheshimiwa Rais Magufuli alisema kuwa atahakikisha katika kipindi cha utawala wake, Serikali inahamia mjini Dodoma, kwa vile Rais wa Awamu ya kwanza Mwl. Julius Nyerere alionesha nia ya kufanya hivyo.

 Aliongeza  kuwa  kwa sasa mji wa Dodoma unaweza kukidhi mahitaji hayo ya Serikali kwa kutumia  miundombinu iliyopo, hata hivyo Serikali inaendelea kujenga miundombinu mipya.

Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa hufanyika Julai 25, ya kila mwaka, kwa   kufanya  maombolezo ya Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali katika harakati za kutetea uhuru wa nchi ya Tanzania.

 Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma, ambapo Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria maadhimisho hayo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.